Kiswahili

Karibu

Habari

Picha ya skrini

Kanuni

Masomo

Pakua

Mwasiliani

Deutsch English Español Français Kiswahili

Karibu

awale huru ni programmu haina bei inapatikana na leseni ya GNU general public licence. Unaweza kuipakua, kuitumia, kuibadili na kuigawa, lakini ni lazima utumie licensi ya GPL.

Programmu hii ya awale huru inatumia kanuni ya "min-max" ya Von Neuman imegeuzwa kidogo. Kanuni hii ni nzuri sana kwa sababu kuna hiari ndogo kila wakati. Ukianza, programmu inachunguza kama zamu 10. Lakini, hesabu ya nambari za zamu inatumia nguvu ya kompyuta yako na urahisi unataka kucheza nayo.

Kwa ukurasa hii, utapata habari ya mchezo wa awale. Hii ni tovuti rasmi wa programmu awale huru. Tovuti ya kutengeneza awale huru ni http://savannah.nongnu.org/projects/awale.

Habari

Unaweza kupata toleo 1.6 sasa

Toleo rasmi ni awale-1.6.

Historia ya toleo

31 Oktoba 2015, toleo 1.6
Tafsiri ya Kijerumani

18 Februari 2012, toleo 1.5
Mbegu zinawekwa pole pole kuonyesha masogea ubainifu.

30 Julai 2009, toleo 1.4
Onyesha mbegu 15 kwa shimo.
Hifadhi hiari yote ya mchezo.
Rekebisha makosa ndogo.

6 Mei 2008, toleo 1.3
Unaweza kutumia kanuni za kawaida.
Hifadhi chaguo ya lugha.
Ongeza mchezo ya mwisho unazunguka.

31 Agosti 2007, toleo 1.2
Ugumu sifuri wa wachezaji wapya umeongezwa, na ugumu ya kwanza umepunguzwa kidogo.
Shimo inachezwa ni kompyuta inakazwa.
Kanuni zimetafsiri kwa Kihispania.

13 Mei 2007, toleo 1.1
Sasa, unaweza kuhifadhi na kufungua faili za michezo, na kucheza tena michezo kuu.

17 Februari 2007, toleo 1.0
Toleo ya kwanza

Mbele ya 2007, toleo 0.x
Toleo ya 0.1, 0.2 na 0.3 ziliandikwa kwa C++, VisualBasic na FORTRAN90. Haiwezi patikana kwa mtandao.

Picha ya skrini

Unaweza kucheza awale huru kwa skrini inaonyesha bao na mbegu. Hapa, kuna picha ya skrini ya Mac OS X, GNU/Linux na Windows.

Mac OS X GNU/Linux Windows


Kanuni

Kanuni ya Ivory Coast

Mchezo ya Awale ina laini mbili, na kila laini ina shimo sita. Mchezaji ana cheza kutoka laini moja. Laini ya juu ni ya kompyuta na laini ya chini ni ya mtu. Shimo hizo zingine ni nyumba, na mbegu zimekamatwa zinawekawa hapo.

Ukianza mchezo, shimo zote iko kwa laini zina mbegu nne.

Wachezaji wanacheza moja kwa moja. Mchezaji mmoja hawezi kuchezi mara mbili, na ni lazima acheze mara yake.

Ukicheza, chukua mbegu yote iko kwa shimo, halafu weka mbegu kwa shimo moja kwa moja ukienda upande wa kushoto, weka mbegu moja kwa shimo. Ukizunguka shimo ya kwanza ikiwa na mbegu 12 au zaidi, usiweke mbegu kwa shimo ulianza nayo.

Unaweza kukamata mbegu kama shimo la mwisho iko kwa laini ya mshindani na shimo in mbegu mbili au tatu ukiweka mbegu yako ya mwisho. Ikiwa shimo ya shimo umekamata ina mbegu mbili au tatu, hizo mbegu zinakamatwa pia. Kama shimo nyuma ya hiyo pia ina mbegu mbili au tatu, zinakamatwa pia. Unaweza kuendele kukamata mbegu kwa shimo nne, kama ziko nyuma ya shimo umekamata mbegu na ina mbegu mbili au tatu, lakini unaweza kukamata mbegu hadi shimo nne, huwezi kukamata mbegu kutoka shimo tano.

Kama mshindani hana mbegu ya kucheza, na wewe unaweza kucheza kumpatia mbegu, ni lazima umpatie mbegu. Kama huwezi kumpatia mbegu, mumemaliza kucheza.

Mshindi ni mtu amekamata mbegu mingi.

Kanuni mbadala

Kuna kanuni tofauti zinatumikana kwa Afrika magharibi. Hapa, tumetumia kanuni za Ivory Coast, lakini Ivory Coast pia, kuna kanuni tofauti zinaweza kutumikana.

Watu wanaweza kutumia kanuni zina sema unwaeza kukamata mbegu kutoka shimo sita.

Another variant is that when you are in position to eat more than four holes and you play it, you eat nothing at all. In this implementation of the game, we have admitted that the maximum number of holes to be eaten is four, and that when more than four holes are eatable, you eat the last four holes.

Kanuni ingine inasema, mshindi hakukamata mbegu ya mwisho. Hatutumia kanuni hii kwa awale huru.

Watu kutoka Afrika magharibi wanacheza kwa haraka. Watu wanaweza kungoja nukta nne ukifikiri, lakini wanapenda sana ukicheza hapo papo. Wanapenda umecheza sana, umeelewa wendo nzuri. Michezo ya kawaida inatumia dakiki kumi.

Pakua

Unaweza kupata faili ya programmu na programmu za GNU/Linux, Mac OS X na Windows kwa http://download.savannah.nongnu.org/releases/awale.

Programmu ya Windows

Pakua programmu na dabiri awale-1.x-w32.exe. Hii itaweka mchezo wa awale huru kwa kompyuta yako. Pia, ni lazima uwe na programmu Tcl/Tk kwa kompyuta yako.

Programmu ya OpenMandriva, CentOS, Redhat

Programmu za OpenMandriva, CentOS, Redhat iko kwa awale-1.x-1.x86_64.rpm. Pakua hii faili, alafu dabiri faili, na itaweka awale huru kwa kompyuta yako.

Programmu ya Debian au Ubuntu

Programmu ya Debian au Ubuntu iko kwa awale-1.6_x86_64.deb (64 bits). Pakua hii faili, halafu dabiri faili na itaweka awale huru kwa kompytua yako.

Programmu ya Mac Intel OS X

Programmu ya Mac OS/X iko kwa faili awale-1.x-macOSX.dmg. Pakua hii faili, fungua diski halafu weka faili awale.app kwa folda Applications.

Sanya-zalisha kwa GNU/Linux systems

Kusanya-halisha programmu ya awale huru kwa kompyuta ya GNU/Linux, pakua awale-1.x.tar.gz halafu toa kwa faili ndogo na
tar -zxvf awale-1.x.tar.gz
ingia folda ya awale-1.x
cd awale-1.x
tengeneza "makefile" na
./configure
Sanya-halisha
make
kwa mwisho sakinisha programmu
make install
Elezo kamilika ya kusakinisha iko kwa faili INSTALL (kwa Kiingereza).

Sanaya-zalisha kwa Mac OS X

Kusanya-halisha programmu ya awale huru kwa kompyuta ya Mac OS X, ya kwanza sakinisha "Xcode development tools" iko kwa diski ya pili ya kusakinisha Mac OS X 2, halafu pakua awale-1.x.tar.gz. Kwa macbook yangu, faili imepanuka, kupata folda
tar -xvf awale-1.x.tar
halafu ingia folda ya awale-1.x
cd awale-1.x
tengeneza "makefile"
./configure --mandir=/usr/local/share/man
sanya-halisha programmu
make
kuwa msimamizi
sudo su
kwa mwisho, sakinisha programmu
make install
kamilika ya kusakinisha iko kwa faili INSTALL (kwa Kiingereza).

Kucheza

Kutumia GUI (skrini na picha) kwa kompyuta ya GNU/Linux systems na Mac OS X, chapa
xawale
kwa sheli. Pia unaweza kutafuta vile watu wanaweka picha kwa mwambaa zana ya kuanza programmu, na kutumia njia hiyo kwa awale huru.

Kucheza awale huru kwa Windows, bonyeza ikoni iko kwa eneo ya kazi.

Kwa kompyuta yote, unaweza kucheza na matini tu, chapa,
awale
Kuona chaguo iko kwa matini tu, chapa
awale -h
au
man awale
Hapa, unaweza kuanza mchezo na mbegu iko pahali yote unataka, unaweza kujaribu mchezo mmoja - inaweza kusaidia ukicheza na mtu mwingine.

Mahitaji

Programmu inatumia picha kwa uonyesho (GUI) imeandikwa kwa Tcl/Tk. Kwa kawaida programmu hii inaptikana kwa kompyuta ya GNU/Linux au Unix. Lakini kwa kawaida haipatikana kwa Windows. Kama haiko kwa kompyuta unatumia, unaweza kuipakua kwa http://www.tcl.tk/software/tcltk.

Mwasiliani

Alain Le Bot , Laurent Le Bot, Diana Martin de Argenta na Christian Gruber wameandika programmu ya Awale. Watu wangependa kusaidia kutengeneza Awale wanakaribishwa.

Ukiona makosa, au vitu tunaweza kufanya kuboresha progammu, tafadhali tuma barua pepe kwa awale-developpeur@nongnu.org

Hakimiliki (H) 2007 Alain Le Bot, Rekebisho ya mwisho 15 Novemba 2015