Kiswahili
Header image

Karibu

Habari

Picha ya Onyesho

Kanuni

Masomo

Pakua

Mwasiliani

English Français Español Kiswahili

Masomo ya Awale huru

Bao

Bao ina laini mbili ya shimo sita. Laini ya juu ni ya mchezaji wa kaskazini, na laini ya chini ni ya mchezaji wa kusini. Shimo hizo zingine zimezungushiwa na rangi nyeusi hazitumuki kwa mchezo. Hizo ni nyumba, zinatumika kuweka mbegu zimekamatwa.

Header image

Mchezo ukianza, shimo zote ina mbegu nne.

Shabaha

Mshindi ni mchezaji ambaye amekamata mbegu zaidi kuliko mpinzani.

Move

Wachezaji wanabadili kucheza. Ni lazima mchezaji acheze mara yake.

Mchezo ukianza, kila shimo ina mbegu nne (picha ya kwanza). Chagua shimo moja, toa mbegu yote na weka mbegu kwa shimo ya upande wa kushoto, mbegu moja kwa shimo.

Kwa zamu baadaye, chukua mbegu iko kwa shimo upande yako, na gawa mbegu. Picha inaonyesha mbegu nne zikigawana kwa shimo nne.

Header image

Unaweza kuweka mbegu kwa upande wako tu, kwa mfano unaweza kucheza kutoka shimo ina mbegu moja tu.

Header image

Kama shimo ya kwanza in mbegu kumi na mbili au zaidi, usiweke mebgu ndani ya shimo la kwanza ukizunguka. Kwa mfano hii, shimo ya kwanza ina mbegu 14 (picha ya kushoto), mbegu ya 12 imewekwa ndani shimo kwa upande wa kushoto wa shimo la kwanza. Picha ya kulia inaoneysha bao baada ya kugawana mbegu. Shimo tatu zimepata mbegu mbili.

Header image Header image

Kukamata

Kama shimo la mwisho iko na mbegu mbili au tatu mchezaji akimaliza kugawana mbegu, mchezaji huyu atakamata hizo mbegu. Picha hizi zinaonyesha mbegu mbili na tatu zimekamatwa.

Header image Header image

Mchezaji anaweza kukamata mbegu kutoka shimo ziki jirani, lakina ni lazima shimo ina mbegu mbili au tatu.

Header image

Kukamata mbegu kutoka shimo ziko zaidi ya moja, ni lazima shimo ziko jirani, kwa mfano, picha hii inaonyesha mebgu zimekamatwa kutoka shimo tatu, lakini shimo ya nne ina mbegu nne, kwa hivyo haiwezekana kukamata mbegu hizo.

Header image

Mchezaji hawezi kukamata mbegu kutoka shimo zaidi ya nne, shimo zingine zinapuuzwa.

Header image

Kupatia chakula

Kama hana mbegu, ni lazima umpatia mbegu.If the opponent has no seed, one must play to feed it. Picha inaonyesha bao ambaye mchezaji anaweza kuchukua mbegu kutoka shimo ina mbegu nne tu.

Header image

Mwisho wa mchezo

Kama mchezaji mmoja hawezi kucheza kwa sababu mbegu zake zimeisha, mchezo umeisha. Mpinzani anaongeza mbegu upande wake kwa jumla yake.

Header image

Watu wanaisha kucheza kama mchezo unazunguka. Picha hizi zinaonyesha mchezo ukizunguka wachezaji wakicheza vizuri. Wachezaji wanaongeza mbegu kwa upande wao kwa jumla wao.

Header image Header image

Krou

Krou ni shimo ina mbegu 12 au zaidi. Shimo ikiwa pahali pazuri, inaweza kuhamia laini ya mpinzani. Hapa, krou ina mbegu 14. Ya kwanza, shimo za mpinzani zinaptiwa mbegu, alafu kwa zunguka ya pili, shimo mbili la mwisho zinakamatwa, na mchezaji anapata mbegu 6.

Header image

Kuzima krou, pengine mpinzani anaweza kutengeneza shimo ina mbegu mbili. Hapa kaskazini anaweza kuweka mbegu moja (picha ya kushoto). Shimo ya krou ina mbegu mbili, na mbegu za krou zikiwekwa, itapata mbegu mbili ingine, kwa hivyo itakuwa na mbegu nne. Kwa hivyo krou haitapata mbegu chochote (picha ya kulia).

Header image Header image

Uma

Uma ni mbinu you kuhamia shimo mbili au zaidi. Hapa, mchezaji wa kaskazini anaweza kucheza mbegu 5 (picha ya kushoto). Baada kucheza, shimo mbili za kwanza ya kaskazi zimehamiwa ni mbegu moja na shimo ina mbegu nne (picha ya kulia).

Header image Header image

Kukama shimo la mwisho

Hapa, kusini anacheza kutoka shimo la mwisho (juu na kushoto). Kaskazi anapatia mbegu zake zote (juu na kulia). Kumaliza, kusini anacheza mbegu mbili (chini na kushoto), anapatia kusini mbegu moja, alafu anakamata mbegu hiyo (chini na kulia).

Header image Header image
Header image Header image

Kucheza pole pole

Peingine, ni nzuri kucheza kwa njia haitapatia mpinzani na mbegu. Hii ni mkakati mzuri ya mwisho wa mchezo, kwa sababu mbegu ni chache. Mchezaji anaweza kucheza mara mbili au zaidi bila kupatia mpinzani mbegu anaweza kukama shimo la mwisho. Hapa, kusini anaweza kucheza mbegu moja mara saba bila kupatia kaskazini mbegu. Kusini akicheza na mbegu tatu, atapatia kaskazini mbegu baada ya kucheza mara mbili.

Header image

Mabadiliko

Unaweza kuchagua mabadiliko ya kanuni kwa orodha ya Hiari na Chagua kanuni

.

Unaweza kuchagua shimo zinaweza kukamatwa kutoka, nne, tano ama tisa. Kwa kawaida ni nne.

Kama shimo zaidi kuliko hizo zinawezwa kukamatwa zinahamiwa, shimo za mwisho zinaweza kukamatwa zinakamatwa. Hii ni kanuni ya kawaida. Lakini, watu wanaweza pia kucheza badiliko ambaye hakuna shimo itakamatwa.

Kwa kawaida, unaweza kukamata mbegu zote za mpinzani, halafu mchezo umeisha. Lakini, kunabadiliko ambaye unaweza kucheza kama utakamata mbegu zote, lakini, hutakamata mbegu na mchezo unanendelea.

Kwa kanuni tofauti, huwezi kucheza kutoka shimo inahamia shimo zote za mpinzani kama una shimo ingine unaweza kucheza. Kama hakuna shimo ingine, unacheza na mbegu zinaweza kukamatwa kama unatumia kanuni zinasema mbegu zinaweza kukamatwa. Kwa picha ya kushoto, shimo ina mbegu nne haiwezi kuchezwa, lakini kwa picha ya kulia, ni lazima shimo ina mbegu nne ichezwe.

Header image Header image

Viungo vya Nje

Kanuni ingine zinapatikana kwa:
http://www.oware.org
http://en.wikipedia.org/wiki/Oware
http://webfacil.tinet.cat

Rudi kwa ukurasa wa kwanza

Hakimiliki (H) 2008 Alain Le Bot, Rekebisho ya mwisho 19 february 2012, Tafsiri Benson Muite 27 Novemba 2020